kumekuwa na tabia ya watu kuomba msaada wa ushauri katika mitandao ya kijamii ukiwemo mtandao wa facebook, huku wakieleza shida zao. jambo hili si baya ila ningeomba kuwaeleza kuwa facebook si mtandao wa kuutegemea sana kutokana na nasaha ambazo nimekuwa nikiziona kwa watu, baadhi wana mzaha wa kutoa ushauri na hata wanaoomba ushauri wenyewe huomba kwa mzaha. wengine wamekuwa wakitoa msaada ambao kwakweli kama mtu ana jambo linalomsibu twaweza kuwa tunaandaa mauti ya watu. mfano mtu anaomba ushauri juu ya matatizo ya magonjwa, mapenzi, migogoro fulani na kushindwa katika jambo fulani, utakuta watu wanalopoka tu. jamani si kila mtu anastahili kutoa ushauri au nasaha. uonapo mtu ameomba ushauri na wewe unakielewa kitu aombeacho ushauri, mwelekeze akufikie au andika namba ya simu.
jambo lingine ni watu wanapost eti admin naomba watu wanishauri, mimi nina tatizo fulani. haieleweki anayeomba ushauri yuko wapi, nje ya hayo picha zinazowekwa au maneno yanayotumika ni ya kimzaha tu ambapo mwelewa akiyaona anapuuza tu.
TUNACHOKIFANYA LEO NI MAANDALIZI YA GHARAMA ZA KESHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni