Alhamisi, 20 Machi 2014

USHAURI NA UNASIHI FARAJA YAKO

kumekuwa na tabia ya watu kuomba msaada wa ushauri katika mitandao ya kijamii ukiwemo mtandao wa facebook, huku wakieleza shida zao. jambo hili si baya ila ningeomba kuwaeleza kuwa facebook si mtandao wa kuutegemea sana kutokana na nasaha ambazo nimekuwa nikiziona kwa watu, baadhi wana mzaha wa kutoa ushauri na hata wanaoomba ushauri wenyewe huomba kwa mzaha. wengine wamekuwa wakitoa msaada ambao kwakweli kama mtu ana jambo linalomsibu twaweza kuwa tunaandaa mauti ya watu. mfano mtu anaomba ushauri juu ya matatizo ya magonjwa, mapenzi, migogoro fulani na kushindwa katika jambo fulani, utakuta watu wanalopoka tu. jamani si kila mtu anastahili kutoa ushauri au nasaha. uonapo mtu ameomba ushauri na wewe unakielewa kitu aombeacho ushauri, mwelekeze akufikie au andika namba ya simu.
jambo lingine ni watu wanapost eti admin naomba watu wanishauri, mimi nina tatizo fulani. haieleweki anayeomba ushauri yuko wapi, nje ya hayo picha zinazowekwa au maneno yanayotumika ni ya kimzaha tu ambapo mwelewa akiyaona anapuuza tu.

TUNACHOKIFANYA LEO NI MAANDALIZI YA GHARAMA ZA KESHO

Jumatatu, 30 Desemba 2013

TUBADILIKE

HABARI WATANZANIA.
Ningependa kuleta mada hii mezani kwenu ili tuweze kuijadili.
kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu ndoa au uchumba kuvunjika mapema, je unadhani ni sbabu zipi changizi na nini kifanyike.
kwa upande wangu nimejaribu kuchunguza na kuona kuwa sisi(wanaume) si wakweli; hivyo tumewafanya wanawake waishi bila kutuamini.
kutokana na mtazamo huo wamejikuta wakifanya  kama ambavyo tunafanya sisi ili kujaribu kuturudisha katika tafakuri.
na kwakuwa wanaume hatupendi kusalitiwa bali kusaliti tumejikuta kuwa walalamikaji na kuvunja uhusiano huku tukisahau kuwa hata sisi ni wasaliti.
Tujaribu kuwa wakweli pale tunapowatongoza mabinti ili waingie katika uhusiano wanaoufahamu.
NANI ALAUMIWE? JADILI UNAVYOELEWA

Ijumaa, 13 Desemba 2013

utambulisho

karibu kwenye blogu yangu na tuendelee kushirikishana taarifa. hii itahusu masuala mbalimbali